Monday, December 21, 2015

OZIL; AELEZA SABABU ZA YEYE KUJIANGUSHA MARA KWA MARA UWANJANI

ozil 2
Mesut Ozil ameahidi kuwa kamwe hutomwona akijiangusha ama akijaribu kumdanganya mwamuzi pindi awapo uwanjani.
Kiungo huyo mchezeshaji, ambaye yuko kwenye kiwango cha juu hivi sasa akielekea kuvunja rekodi ya gwiji wa klabu hiyo Thierry Henry kwa kutoa pasi za magoli kwa msimu, tayari ameshatoa pasi za magoli 13 mpaka sasa.
Huku baadhi ya wanasoka wakubwa ulimwenguni wakisifika kwa vitendo vya kujiangusha, na Cristiaono Ronaldo akiwa miongoni mwao, Ozil amekuwa akisifika sana kwa aina yake ya mchezo kwa kutojiangusha hovyo lakini vilevile kutokuwa mchoyo awapo uwanjani.
Hivyo basi, Ozil amefichua siri ya kuwa hivyo na kusema kwamba hali hiyo imetokana na mazoea aliyojijenge awakati akiwa katika umri mdogo kutokana na kucheza katika viwanja ambavyo haikuwa rahisi kujiangusha kwa sababu ya ubora mdogo wa viwanja hivyo.
“Inanifanya nijisikie vizuri sana kusikia hizo taarifa. Hivyo ndivyo nilivyo”, alisema Ozil wakati akiongea na The Times.
“Nimekuwa katika hali hiyo, siku zote nimekuwa mkweli uwanjani. Sitabadilika, sijiangushi, kamwe siwezi kufanya hivyo. Wakati naanza kucheza soka nilikuwa nikicheza katika uwanja mgumu sana, na nisingeweza kujiangusha hovyo kutokana na kuhofia kuumiza miguu yangu. Katika baadhi ya maeneo kulikuwa na mawe”.
“Ndiyo maana hatukuwa tukijiangusha hovyo, kamwe hatukujifunza kujiangusha. Hatukuwa na uwanja ambao ungesapoti sisi kujiangusha. Na hata kwenye viwanja vyenye nyasi bora pia najitahidi sana

Saturday, December 19, 2015

TFF KUMFIKISHA MURO KWA PILATO KWA KAULI ZA KIBAGUZI DHIDI YA MSEMAJI WA SIMBA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litamfikisha kwenye Kamati ya Maadlili mapema Mwakani baada ya sikukuu ya mwaka Mpya 2016, Mkuu wa Mawasiliano wa klabu ya Yanga, Jerry Muro kutokana na kauli zake za kibaguzi dhidi ya Mkuu wa Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara.
Muro alimshambulia kwa maneno ya kibaguzi Manara wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika mkutano uliofanyika jana makao makuu ya klabu ya Yanga jijini Dar es Salaam.
Kauli ya Muro dhidi ya Manara ni kinyume na Katiba ya TFF, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambao zinapiga vita vitendo vya ubaguzi wa aina yoyote katika mpira wa miguu.
Mapema mwaka huu, Muro alifikishwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kutokana na kumshambulia na kumdhalilisha kupitia vyombo vya habari aliyekuwa Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Fatma Abdallah. Kamati ya Nidhamu ilimwadhibu kwa kumpiga faini ya sh. milioni 5.

YANGA MBELE KWA MBELE

KAM

YANGA YALALAMIKIA SIMBA NA AZAM KUBEBWA NA TFF KWENYE LIGI

Jerry Muro pia ametumia mkutano huo kutambulisha wachezaji wapya wa Yanga SC, kulia ni Issoufou Boubacar Garba kutoka Niger

Baada ya jana azam na simba kulalamikia yanga kubebwa kwenye swala la usajili wa ligi kuu bara yanga nayo yaibuka  na malalamiko kuwa timu hizo zinabebwa na tff.
YANGA SC imelalamikia kuchezeshwa mfululizo mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wakati wapinzani wao, Azam FC na Simba SC hawachezi.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro amewaambia Waandishi wa Habari katika Mkutano uliofanyika makao makuu ya klabu Jangwani, Dar es Salaam kwamba hawapendezewi na mwenendo huo.  
“Tunakwenda kucheza kesho na Stand United, lakini wenzetu bado wana viporo na hawachezi. Hizi ni figisu, ilifaa wote tucheze pamoja.
Wakiendelea kufanya hivi, tutatumbua majipu,”. “Kwa nini tuachiwe sisi tu tucheze wakati wenzetu wakae watutazame, si jambo zuri. Tuwaombe wenye kusimamia kanuni na sheria za mpira Tanzania waliangalie hili,”amesema Muro.
Yanga SC inatarajiwa kushuka dimbani kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana na Stand United ya Shinyanga ukiwa ni mchezo wa tatu ndani ya siku 10, baada ya Jumamosi iliyopita kutoa sare ya 0-0 na Mgambo JKT na Jumatano kushinda 1-0 dhidi ya African Sports Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. 
Wapinzani wa Yanga SC katika mbio za ubingwa, Azam FC walimenyana baina yao Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kutoa sare ya 2-2, lakini katikati ya wiki walikuwa mapumzikoni, ingawa kesho nao watakuwa kazini tena.
Azam FC watakuwa Uwanja wa Majimaji Songea kumenyana na wenyeji, Majimaji wakati Simba SC watakuwa wageni wa Toto Africans Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza. 
Jerry Muro pia ametumia Mkutano huo kuwatambulisha wachezaji wapya wa Yanga SC, Paul Nonga kutoka Mwadui FC na Issoufou Boubacar Garba kutoka Niger.